Tumejipanga kufunga hesabu za ubingwa mapema - Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Nov 2021
Tumejipanga kufunga hesabu za ubingwa mapema - Manara

Msemaji klabu ya Yanga Haji Manara amewaambia wale wanaodhani kuwa kasi waliyoanza nayo msimu huu itapoa, watasubiri sana kwani wamejipanga kufunga hesabu katika mbio za ubingwa mapema

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Manara alisema ameyasikia maneno ya watu wanaofananisha mafanikio ya Yanga kwenye duru ya kwanza msimu uliopita na walivyoanza msimu huu

"Kuna watu wanasema hata msimu uliopita tulianza hivi hivi lakini tukapoteza nguvu kwenye duru ya pili, msimu huu wasitarajie hilo"

"Sisi tunaamini huu ndio wakati wetu wa kufunga hesabu katika mbio za ubingwa hatusubiri mpaka michezo ya mwisho. Tumejipanga kwelikweli na tutahakikisha tunakamilisha malengo," alisema Manara

Akizungumzia mchezo unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa kesho katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Manara amesema wanawaheshimu Ruvu Shooting, ni timu nzuri ambayo pia ina kocha mzuri, Charles Boniface Mkwasa ambaye anaifahamu vizuri Yanga

"Tunawaheshimu Ruvu Shooting, ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri na kocha Mkwasa anayeifahamu vyema Yanga. Lakini msimu huu tunaΒ  jambo letu, tunazihitaji alama zote tatu ili tuweze kufikisha pointi 15"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’