Kwetu shabiki ni mchezaji wa kikosi kinachoanza - Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Oct 2021
Kwetu shabiki ni mchezaji wa kikosi kinachoanza - Manara

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Haji Manara amesema ili kuiongezea timu nguvu kuelekea mchezo dhidi ya Azam Fc, mashabiki wanapaswa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao siku ya Jumamosi

Manara amesema shabiki wa Yanga sio mchezaji wa 12, bali ni mchezaji anayeanza kwenye kikosi cha kwanza akiwa jukwaani, umuhimu wake ni wa kipekee

"Haipo namna yoyote ya kushinda Jumamosi bila nguvu ya Washabiki wetu ,tunawahitaji kwa kila hali"

"Mshabiki wa Young Africans sio mchezaji wa kumi na mbili ni Mchezaji wa kikosi kinachoanza akiwa jukwaani, ana umuhimu mkubwa kwetu"

"Chonde Chonde Mwanayanga mwenzangu nunua sasa ticket yako ili tukazisake Points tatu muhimu kwa Mkapa weekend hii," alisema Manara

Tiketi kuelekea mchezo dhidi ya Azam Fc zilianza kuuzwa jana katika vituo mbalimbali pamoja na mitandao ya simu

Nae Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema mashabiki watakuwa na nafasi ya kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kabla ya mchezo

Utaratibu huu watauendeleza kwa mechi zao zote watakazocheza nyumbani

"Mechi zetu zote zitakuwa na wasanii haitaishia hii na Azam Fc kwasababu tuna wasanii wengi sana. Sisi hatutaki shabiki wetu aje uwanjani saa 8:00 mchana achezee simu mpaka iishe chaji badala yake atapata burudani ya wasanii," alisema Bumbuli

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’