Jesus Moloko, Yannick Bangala na Shabani Djuma wanawaalika Wananchi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumamosi, Oktoba 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Hupaswi kukosa burudani ya watu hawa na wenzao pale uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi
Baada ya mechi tatu, ni wazi Yanga ndio timu inayopendeza kuingalia zaidi inapocheza kuliko wengine wote
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Haji Manara anasema Wananchi kupiga pasi 60 mfululizo katika mechi moja kwao ni jambo la kawaida
"Shekhe una Bangala, Aucho na Faeisal pale kati, unakosaje burudani hii...!"
Baada ya Polisi Tanzania kupoteza mchezo dhidi ya Simba jana, Wananchi wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kabla ya kuumana na Azam Fc
Jumamosi wamedhamiria kuendelea kujichimbia kileleni kwa kuibuka na ushindi
Inawezekana kabisa Wananchi watabakia katika nafasi hiyo mpaka mwezi May mwakani....!