Bumbuli awatahadharisha Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Oct 2021
Bumbuli awatahadharisha Azam Fc

Kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Oktoba 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wamepania kuendeleza wimbi la ushindi huku akiwatahadharisha Azam Fc kuwa wajiandae 'kisaikolojia'

Bumbuli amesema wanafahamu mara nyingi mechi zao dhidi ya Azam Fc zinakuwa na upinzani mkali lakini kwa ubora wa kikosi walichonacho msimu huu, wana kila sababu ya kuibuka na ushindi

"Kuna watu wananiuliza eti mnaingia na tahadhari gani kwenye mechi yenu na Azam, hivi sisi Yanga ndiyo tuingie kwa tahadhari kweli? Mimi nadhani Azam ndiyo wanatakiwa kuingia kwa tahadhari kwenye mechi dhidi yetu. Wanatakiwa wawe na tahadhari la sivyo wanaweza kupigwa mabao mengi," alitamba Bumbuli

Bumbuli amesema mchezo huo hautakuwa tofauti na mechi nyingine ambazo Yanga wamecheza mpaka sasa kwani kila timu inapokutana na Yanga inakuwa ni fainali

"Hata hao Azam, wakicheza dhidi ya Yanga ndiyo wanaachia silaha zao zote. Watapambana kwa kila hali na makocha wetu wanalijua hilo. Ila tunawaambia Azam wajiandae maana sisi hatuna uwanja mgumu, mwepesi, mzuri wala mbaya zitakuwa zinaguswa tu. Na kama kuna mtu anatakiwa kufukuzwa basi wafanye hivyo mapema ili isije kuonekana Yanga ndiyo sababu ya kufukuzwa kwake!"

Yanga inatarajiwa kurejea mazoezini kesho Jumamosi kuanza maandalizi ya mchezo huo ambao umerejeshwa uwanja wa Benjamin Mkapa awali ukipangwa kupiga uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’