Mayanga amuengua Kakolanya kikosi cha Stars

Admin By Admin
•
10 Jul 2017
Mayanga amuengua Kakolanya kikosi cha Stars
Golikipwa wa Yanga Beno Kakolanya ametemwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kitakachoivaa Rwanda kwenye mchezo wa awali kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya CHAN dhidi ya Rwanda Julai 15.

Kakolanya alipata majeraha nchini Afrika Kusini.

Kocha Salum Mayanga amemteua mlinda lango wa Serengeti Boys Ramadhani Kabwili kuchukua nafasi ya kakolanya.

Taifa Stars wataanza kampeni za kuwania kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee kwa mara ya pili baada ya mwaka 2009 nchini Ivory Coast kwa kumenyana na Amavubi Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Na baada ya kurejea jana nchini na ushindi wa tatu kwenye michuano ya Kombe la COSAFA Castle nchini Afrika Kusini, kocha Mayanga anayesaidiwa na Fulgence Novatus amefanya mabadiliko madogo kikosini.

Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Mayanga amesema kikosi cha wacheaji 24 kitaondoka leo jioni kwenda Mwanza kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.

“Leo jioni tunatarajia kuondoka kuelekea mjini Mwanza kwa ajili ya kuweka kambi kwa muda wa takribani siku nne kujiandaa na kufanya mazoezi ya kutosha ili tarehe 15 tufanye vizuri katika mechi dhidi ya Rwanda,”amesema kocha huyo na mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Kikosi kinachotarajiwa kuondoka leo kinaundwa na makipa Aish Manula, Said Mohammed na Ramadhani Kabwili.

Mabeki; Shomari Kapombe, Hassan Kessy, Gardiel Michael, Hamimu Abdul, Boniface Maganga, Salim Mbonde, Abdi Banda na Nurdin Chona.

Viungo; Muzamil Yassin, Himid Mao, Salmin Hoza, Raphael Daud, Erasto Nyoni, Said Ndemla, Simon Msuva, Shiza Kichuya na Joseph Mahundi.

Washambuliaji ni Athanas Mdamu, John Bocco, Kelvin Sabato na Stahmil Mbonde.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
5m ago
READ MORE →
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
2h ago
READ MORE →
Kapteni Beka mbioni kurejea kikosini
Kapteni Beka mbioni kurejea kikosini
3h ago
READ MORE →
Kituo kinachofuata ni Kagera Sugar
Kituo kinachofuata ni Kagera Sugar
5h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
9h ago
READ MORE →
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
21h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1d ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1d ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1d ago
READ MORE →