Wananchi wanaondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea Songea kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa keshokutwa Jumanne katika uwanja wa Majimaji
Yanga inakwenda Songea kwa kutumia usafiri wa ndege (ATCL) ikiwa na kikosi kitakachojumuisha wachezaji 24 na viongozi wa benchi la ufundi
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amesema wanakwenda Songea wakiwa na dhamira ya kuhakikisha wanashinda na kurejea nyumbani na alama zote tatu
Baada ya mchezo huo Yanga itarejea Dar kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Oktoba 30
Awali mchezo huo ulipangwa kupigwa mkoani Arusha lakini sasa umerejeshwa kunako uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya maoni ya Wanachama na Mashabiki wa Yanga
ADVERTISE HERE