URA imetinga fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya Yanga katika mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana katika dakika 90.
Mchezo huo ulikuwa mgumu kwa kila upande kutokana na uimara wa safu za ulinzi za timu zote.
Kanuni za michuano hiyo zinabainisha kuwa hakutakuwa na muda wa ziada kama timu zitakwenda sare katika muda wa dakika 90 za kawaida hivyo kupelekea kwenda moja kwa moja kwenye changamoto ya mikwaju ya penati.
URA ilifunga penati zake zote tano huku Yanga ikikosa penati moja iliyopigwa na Obrey Chirwa.
Papi Tshishimbi, Gadiel Michael, Hassan Kessy na Raphael Daudi wote walifunga mikwaju yao.
Lolote linaweza kutokea katika changamoto ya mikwaju ya penati, hivyo licha ya kufungwa kwa matuta, kikosi cha Yanga kinahitaji pongezi kwa upiganaji waliouonyesha katika mchezo huo.
Kikubwa cha kujivunia ni faida kubwa iliyopata Yanga kutokana na michuano hiyo.

ADVERTISE HERE