Katika mwendelezo wa maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya KMC, Jumapili ya wiki hii kikosi cha Yanga kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU kutoka visiwani Zanzibar
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuanzia saa moja usiku
Azam TV watakuwa mbashara kupitia Azam Sport 1 HD
Huu ni mchezo ambao utawapa nafasi wachezaji ambao hawakutumika sana kwenye kikosi cha kwanza na wale waliopona majeraha karibuni
Mapinduzi Balama, Yassin Mustafa na David Bryson ni miongoni mwa wachezaji hao
ADVERTISE HERE