Tanzania imepoteza mchezo muhimu nyumbani baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Benin katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la Dunia
Ulikuwa mchezo ambao Tanzania ingeweza kufunga mabao zaidi ya matatu kama wachezaji wake wangekuwa na umakini
Tanzania ilizihitaji sana alama hizi tatu katika kampeni yake ya kuwania kufuzu kombe la Dunia
Vijana wa Kim Poulsen wanahitaji kushinda mchezo wa marudiano kule Benin ambao utapigwa Oktoba 10
Tanzania inaondoka kesho Ijumaa kuelekea Benin



ADVERTISE HERE