Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Oktoba 30,wameomba uchezwe uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha
Bumbuli amesema wamefikia uamuzi huo ili kuwapa burudani wapenzi na Wanachama wao wa mkoani Arusha
Mwishoni mwa msimu uliopita mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam kati ya Simba dhidi ya Yanga ulipigwa mkoani Kigoma, huo ndio mchezo mkubwa zaidi wa dabi
Bumbuli amesema uongozi wa Yanga umeona waipeleke mechi hiyo ya pili kwa ukubwa kwa mashabiki wao Arusha
ADVERTISE HERE