Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema lengo la kupata alama tatu dhidi ya Kagera Sugar wamelifanikisha na sasa wanahamshia mawazo yao kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya Geita Gold utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 02 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Jana Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopigwa uwanja wa Kaitaba
Kaze amesema wataendelea kukijenga kikosi na timu itazidi kuimarika sasa wakielekeza nguvu zao katika mchezo unaofuata
"Mechi ya kwanza ya ligi, ushindi ugenini, tunaendelea kujenga timu na tutaimarika zaidi. Mechi inayofuata inakuja siku 3 mbele, Oct 2nd dhidi ya Geita Gold, tuko nyumbani," aliandika Kaze kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo dhidi ya Geita Gold