Yanga imefanikiwa kuondoka na alama zote tatu dhidi ya Kagera Sugar baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Kaitaba
Feisal Salum 'Fei Toto' ndiye aliyeihakikishia Yanga ushindi muhimu baada ya kufunga bao pekee kwenye dakika ya 24 akimalizia mpira ambao uliokolewa na mlinda lango wa Kagera Sugar baada ya shuti la Fiston Mayele
Yanga watajilaumu wenyewe kwa kukosa kuibuka na ushindi mnono zaidi kwani walitawala na kutengeneza nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza
Kipindi cha pili Kagera Sugar waliimarika na kupeleka mashambulizi katika lango la Yanga
Lakini uimara wa safu ya ulinzi iliyokuwa chini ya Yannick Bangala na Dickson Job, wakishirikiana na mlinda lango Djigui Diarra, walihakikisha wanaondoa hatari zote langoni
Akizungumza baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema hakufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake hasa katika kipindi cha pili
Hata amesema vijana wake wametoka kucheza mechi ngumu dhidi ya Simba siku tatu zilizopita, imechangia 'kukata' upepo katika kipindi cha pili
Ni alama tatu muhimu kwa Yanga ambazo zinawafanya kuwa miongoni mwa timu zilizoshinda katika raundi ya kwanza



