Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wachezaji Saido Ntibazonkiza, Dickson Ambundo sio miongoni mwa wachezaji waliosafiri na timu mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Jumatano katika uwanja wa Kaitaba
Bumbuli amesema Ambundo ni majeruhi, aliumia mazoezini wakati Saido naye bado hayuko fiti kwa asilimia 100
Aidha Bumbuli amesema benchi la ufundi liliona hakuna sababu ya kusafiri na wachezaji ambao hawatatumika Jumatano
Kiungo Mapinduzi Balama pia amebaki akiendelea kuimarika baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje mwaka mzima wakati Mukoko Tonombe anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Simba msimu uliopita
Mukoko alikosa mchezo wa Ngao ya Jamii juzi na atakosa michezo mingine miwili ya ligi ambayo ni dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold
"Saido Ntibazonkiza , Dickson Ambundo na Mapinduzi Balama hawasafiri na timu kwasababu hawana utimamu wa mwili Ambundo aliumia mazoezini Hauwezi kusafiri na wachezaji ambao hautaweza kuwatumia ndiyo maana hata Mukoko hayupo na Kikosi na atakosekana pia kwenye mchezo wetu wa nyumbani dhidi ya Geita Gold," alisema Bumbuli
Yanga imewasili Bukoba mapema leo tayari kwa mchezo huo wa kwanza msimu huu