Baadhi ya vyombo vya habari vinaripoti kuwa winga Deus Kaseke anakaribia kutua Singida United baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika.
Katibu Mkuu Charles Mkwassa amesema Kaseke ni miongoni mwa wachezaji walio kwenye mipango ya kocha George Lwandamina na tayari mazungumzo ya kumuongeza mkataba wa miaka miwili yalishafanyika kilichokuwa kinasubiriwa ni kusaini tu.
Sasa baada ya kuripotiwa kwa taarifa kuwa Singida United inamnyemelea, Uongozi umemsafirisha haraka jijini Dar es salaam ili asaini mkataba wa kuendelea kubaki Jangwani.
Kaseke pia anatakiwa kujiunga na kikosi cha Yanga kinachotarajia kuanza maandalizi ya msimu mpya mwanzoni mwa wiki ijayo.
Kocha wa Singida United, Hans van Pluijm kuna wachezaji anawatamani kutoka kikosi cha Yanga, Kaseke ni miongoni mwao.
Kaseke ana faida kubwa kwenye timu kwa kuwa anaweza kucheza nafasi zaidi ya moja.
Mchezaji mwingine ambaye hatutashangaa akitua Singida United ni Deogratius Munishi 'Dida' ambaye licha ya kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio, upo uwezekano akarudi kuitumikia timu hiyo kama atashindwa.
Yanga tayari imeshafanya mchakato wa kusajili golikipa mwingine hivyo hahitajiki tena kulingana na taarifa iliyotolewa na kocha wa makipa Juma Pondamali.

ADVERTISE HERE