Mayele ni hatari sana - Kocha DTB

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Sep 2021
Mayele ni hatari sana - Kocha DTB

Juzi DTB inayoshiriki ligi daraja la kwanza, ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga, mchezo ukipigwa Avic Town, Kigamboni

Yanga iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, wafungaji wa mabao ya Yanga wakiwa Fiston Mayele, Yusufu Athumani na Bryson David

Ulikuwa mchezo wa pili DTB inaumana na Yanga na matokeo yakiwa sawa katika michezo yote miwili, Mayele akifunga katika kila mchezo

Kocha Mkuu wa DTB Ramadhan Nsanzurwimo amemtaja mshambuliaji Fiston Mayele kuwa mchezaji hatari ambaye ataisaidia sana Yanga msimu huu

Nsanzurwimo amesema mashabiki wa Yanga watarajie makubwa kutoka kwa Mcongomani huyo lakini timu pinzani zijipange kwelikweli kukabiliana nae

"Nimekiangalia kikosi cha Yanga na nawaambia mashabiki wa timu hiyo watarajie makubwa sana kwa mshambuliaji wao mpya, Fiston Mayele kwani kwa jinsi alivyo wapinzani wajipange"

"Nimemshuhudia Mayele akiisaidia Yanga kwenye mechi za kirafiki tulizocheza na Yanga, nawatahadharisha timu nyingine za ligi Kuu Bara msimu huu"

"Mayele ni mchezaji msumbufu sana na anayeweza kucheza kwa nafasi, unaweza usione madhara yake lakini anajua kucheza na akili za mabeki," alisema Nsanzurwimo

Mayele ameifungia Yanga mabao manne katika michezo yote ya kirafiki iliyofanyika Avic Town

Hakutumika katika mechi za ligi ya mabingwa kwa kuwa ITC yake ilifika Yanga nje ya muda wa usajili wa dirisha la CAF

Yanga itamtumia Mayele katika michuano yote ya ndani ikiwemo Ngao ya Jamii, Ligi Kuu, Kombe la FA, Kombe la Mapinduzi n.k

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’