Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe ameondoka Zanzibar leo kurejea Dar es salaam kupata matibabu zaidi baada ya kukumbwa na malaria.
Tambwe amekuwamo kwenye kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya kombe la Mapinduzi lakini ameshindwa kucheza hata mchezo mmoja kutokana na kusumbuliwa na malaria kwa takribani siku nne.
Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu amethibitisha kuondoka kwa Tambwe kurejea Dar es salaam.
"Ana malaria,kwa siku zaidi ya nne sasa amekuwa na wakati mgumu, tumelazimika kumrejesha Dar ili apate matibabu zaidi" amesema Dr Bavu.
Yanga tayari imetinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi leo ikitarajiwa kucheza mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya Singida United.

ADVERTISE HERE