Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka mapema jijini Dar es salaam kuelekea Nigeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United
Mchezo huo wa mkondo wa pili, utapigwa Jumapili ijayo Septemba 19, Port Harcourt
Taarifa za ndani zimebainisha kuwa Yanga itaondoka nchini kwa usafiri wa ndege ya kukodi ili kuhakikisha wachezaji wanafika mapema na pia timu inarejea mapema kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 25
Yanga inahitaji kupata ushindi wa angalau mabao mawili ili kuweza kufuzu raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa
Hakuna lisilowezekana kwenye mpira wa miguu
ADVERTISE HERE