Yanga imepoteza mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa wakimkubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Rivers United ya Nigeria
Bao pekee la Rivers United lilifungwa na Moses kwenyye dakika ya 51 kwa mpira wa kichwa
Ulikuwa mchezo ambao pengine Yanga itajilaumu kwa kushindwa kutumia nafasi nyingi walizotengeneza hasa katika kipindi cha kwanza
Makosa katika safu ya ulinzi yameigharimu Yanga, sasa wakiwa na kazi ya ziada kwenda kusaka matokeo kule Nigeria
Yacouba Songne, Feisal Salum na Yusufu Athumani wataziota nafasi muhimu walizozipoteza katika mchezo huo
Kwa hakika ni siku mbaya kwa Wanayanga waliokuwa na matumaini makubwa kwa timu yao siku ya leo
Kocha Nasreddine Nabi ana wiki moja ya kuwaandaa vijana wake kwa ajili ya mchezo wa marudiano kule Nigeria
Β