Kikosi cha Yanga leo majira ya saa 11 jioni kitashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Rivers United katika mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali
Baada ya kukosa kushiriki michuano ya Kimataifa kwa msimu uliopita, Yanga inarejea katika michuano ya ligi ya mabingwa ikiwa na malengo ya kufanya vizuri zaidi
Ni mchezo ambao Yanga inahitaji kupata ushindi mnono ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutinga raundi ya kwanza katika mchezo wa marudiano ambao utapigwa wiki ijayo Nigeria
Yanga imekuwa kwenye maandalizi makali kwa takribani wiki mbili, timu ikiingia kambini mara baada ya mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Zanaco Fc August 29
Mchezo utapigwa pasipo uwepo wa mashabiki Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) likizuia mashabiki katika mechi hizi za hatua ya awali
Kikosi cha Yanga kiko imara na tayari kuwapa furaha mashabiki wake licha ya kuwakosa wachezaji Shabani Djuma, Khalid Aucho na Fiston Mayele ambao ITC zao hazikufika kwa wakati
Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema wako tayari kuibuka na ushindi leo akiwataka mashabiki kuiombea duwa timu yao ili iweze kupata matokeo mazuri
Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga kushinda ili kuweza kutimiza malengo yake. Katika michuano ya ligi ya mabingwa, Yanga imelenga kuvuka hatua ya makundi
Kila la kheri Wananchi...!