Aliyewahi kuwa kocha wa Yanga Cedric Kaze alipendekeza usajili wa mlinzi wa kati Dickson Job kwa kamati ya Ufundi ya Yanga iliyokuwa ikiongozwa na Dominic Albinus 'Baba Paroko'
Albinus amebainisha jambo ambalo Kaze alimueleza kwa nini anamuhitaji mlinzi huyo licha ya Yanga kuwa na walinzi wengine mahiri wa kati
"Ninahitaji mumsajili Dickson Job kwasababu ni beki mwenye footwork nzuri," kauli ya Kaze
Kaze alikuwa anataka beki wa kati anayeweza kucheza mpira. Bahati mbaya Kaze aliondoka kabla Job hajakanyaga uwanjani akiwa na uzi wa Yanga. Ila kama anatazama mechi za Yanga, labda moyo utakuwa umesuuzika.
Falsafa ya kocha Nabi, Yanga wanahitaji kucheza kuanzia nyuma, ndio maana pasipo shaka jina la Dickson Job litakuwa la kwanza kwenye karatasi ya kocha huyo.
Dickson Job ni mtulivu, yupo 'comfortable' sana akiwa na mpira mguuni. Anapopokea pasi, anatulia na kuangalia sehemu sahihi zaidi ya kuicheza.
Job pia ni mchezaji mwenye UJASIRI nyuma ya moyo wake. Hata katika nyakati alizowekwa katika shinikizo bado alithubutu kutulia na kufanya maamuzi.
Yanga Ina mabeki wengi na wazuri, wana vitu kadhaa zaidi kumzidi Job lakini kuhusu kucheza mpira, nafikiri Dickson Job ni bora zaidi yao.
Nasubiri kumuona Job zaidi chini ya kocha Nabi. Kocha yeyote anayependa kucheza soka la pasi fupi kuanzia nyuma, jina la Dickson Job litakuwa la kwanza kwenye safu ya ulinzi ya Yanga.
Akiwa kijana mdogo aliyepita ngazi zote za timu za Taifa naamini ni nguzo na tegemeo kwa timu yake ya Yanga na Taifa stars kwa miaka mingi sana.
Wengi wamekuwa na hofu na kimo chake,ila ukifuatilia vizuri ni mchezaji anayefanya vizuri sana hasa linapokuja swala la kuwania mipira ya juu dhidi ya washambuliaji warefu.
Amekuwa akitumia akili kubwa na timing ya hali ya juu kuiwahi mipira yote ya juu katika eneo lake
Kwa hisani ya Baba Paroko