Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' jioni ya leo kitashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Madagascar katika mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki kombe la dunia Qatar 2022
Baada ya kufanikiwa kupata alama moja kule DR Congo kwa sare ya bao 1-1, Stars ina nafasi ya kupanda kileleni mwa kundi J kama itapata ushindi dhidi ya Madagascar
Jana Benin na DR Congo zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bao 1-1
Benin wanaongoza wakiwa na alama nne, wakifuatiwa na DR Congo wenye alama mbili timu zote zikiwa zimecheza michezo miwili
Tanzania iko nafasi ya tatu ikiwa na alama moja wakati Madagascar walipoteza mchezo wao wa kwanza kwa kufungwa na Benin bao 1-0 hivyo hawana pointi
Mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa kumi kamili jioni, hautahudhuriwa na mashabiki
Stars leo itakuwa na nahodha wake Mbwana Samatta ambaye alikosa mchezo wa kwanza kule DR Congo akishuhurikia uhamisho wake nchini Ubelgiji