Yanga Princess imeongeza wachezaji wawili katika kikosi chake kitakachowania ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite' msimu huu
Mshambuliaji hatari wa JKT Queens Asha Rashid Mlangwa maarufu Mwalala ametua akitarajiwa kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji inayoongozwa na mfungaji bora wa msimu uliopita Aisha Masaka
Aidha Yanga Princess pia imefanikiwa kumnasa mshambuliaji Daniela Kanyanya Ngoi ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya DR Congo
Kikosi cha Yanga Princess ambacho sasa kiko chini ya kocha Mohammed Hussein 'Mmachinga', hakina mabadiliko makubwa baada ya kufanikiwa kuwabakisha mastaa wake wote wakiwemo manahodha Happyness Mwaipaja na msaidizi wake Amina Bilali pamoja na Masaka waliokuwa wakisakwa na timu mbalimbali
Nyota wengine ambao wataendelea kuwepo kwenye kikosi cha Yanga Princess ni Aisha Juma Bulebule, Anastazia Nyandago, Aniella Uwimana, Asphat Kasindo, Belina Julius, Clara Luvanga, Emeliana Mdimu na Fatuma Makusanya
Wengine ni Fatuma Mwisendi, Fumukazi Ally, na Husna Mtunda. Wanaungana ni Irene Kisisa, Janeth Pangamwene, Lucia Mrema, Neema Chibara, Noela Luhala, Olga Kalamba, Pheromena Daniel, Tausi Swalehe na Zulfa Makau
Jeshi la Yanga Princess litakuwa na wachezaji 25