Said Mussa akimbizwa Hospitali kuchunguzwa mkono

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jan 2018
Said Mussa akimbizwa Hospitali kuchunguzwa mkono
Uongozi wa Yanga umesema umelazimika kumkimbiza Hospitalini winga Said Mussa baada ya kuumizwa mkono kwenye mchezo wa kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa ya Jan'gombe jana.

Mussa alitolewa kwenye dakika 75 na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi baada ya kufanyiwa madhambi mfululizo.

Katika mchezo huo ambao Yanga ilitinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, takwimu zinaonyesha Said Mussa ndiye mchezaji aliyefanyiwa madhambi zaidi.

Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu amesema Mussa amemka leo akiwa na maumivu makali ya mkono, huku ukiwa na uvimbe kwenye mkono huo.

"Awali tulijua ni tatizo dogo lakini asubuhi mkono umeamka umevimba sana na tumelazika kumkimbiza hospital baada ya hapa tutatoa taarifa nyingine," amesema Dk Bavu.

Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa alimlalamikia mwamuzi juu ya rafu mbaya zilizokuwa zinafanywa na wachezaji wa Taifa lakini hakutoa adhabu yoyote kali zaidi ya kadi ya njano.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’