FT : Yanga 1-2 Zanaco Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Aug 2021
FT : Yanga 1-2 Zanaco Fc

Mchezo wa kuhitimisha kilele cha wiki ya Mwananchi kati ya Yanga dhidi ya Zanaco Fc umemalizika kwa wageni kupata ushindi wa mabao 2-1

Ulikuwa mchezo wa kwanza wa ushindani kwa kikosi cha Yanga ambacho kimesukwa upya

Heritier Makambo aliitanguliza Yanga bao safi kwenye dakika ya 31 akifunga baada ya kuwaramba chenga walinzi wa Zanaco Fc

Hata hivyo Zanaco walirejea mchezoni kwenye kipindi cha pili na kufanikiwa kupata mabao yao mawili

Akizungumza baada ya mchezo huo, Razack Siwa, kocha wa makipa aliwatoa wasiwasi mashabiki wa Yanga akiwahakikishia kuwa timu itakaa sawa

Yanga imekuwa na changamoto katika maandalizi yake ambapo walilazimika kusitisha kambi nchini Morocco kutokana na joto kali pamoja na baadhi ya wachezaji kutakiwa kujiunga na timu za Taifa

Ilifanya mazoezi Morocco kwa takribani siku tano huku wachezaji wengine tisa wakirejea nchini jana

Kocha Nasredine Nabi atakuwa na wiiki mbili za kukiweka sawa kikosi chake kabla ya kuanza ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United Septemba 12

Wachezaji wapya wameonyesha uwezo wao, Jesus Moloko, Shabani Djuma, Yannick Bangala, Heritier Makambo, Fiston Mayele bila ya kumsahau mlinda Djigui Diarra aliyekuwa bora sana langoni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’