Hiyo 'battle' ya eneo la kiungo usipime

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Aug 2021
Hiyo 'battle' ya eneo la kiungo usipime

Usajili wa kiungo Khalid Aucho umeongeza ushindani katika eneo la kiungo ndani ya kikosi cha Yanga

Msimu uliopita katika eneo hilo, Kocha Nasreddine Nabi aliwategemea zaidi Mukoko Tonombe, Zawadi Mauya na Feisal Salum 'Fei Toto'

Wakati Nabi akimbadilishia majukumu Feisal kwa kumsogeza eneo la ushambuliaji, ushindani utakuwa mkubwa kati ya viungo wakabaji Mauya, Mukoko na Aucho

Kwani kati yao, ni wawili tu watakaokuwa wakianza kwenye kikosi cha kwanza kwa kuzingatia aina ya mfumo ambao Nabi hupendelea kuutumia

Viungo hao wote wameitwa timu za Taifa, Mauya akiwa kwenye kambi ya Taifa Stars, Mukoko anaelekea DR Congo na Aucho yuko Uganda

Katika moja ya mahojiano yake wakati Yanga ikiwa kambini Morocco, Mukoko alisema msimu ujao ushindani utakuwa mkubwa kwani hakuna mchezaji atakayekuwa na uhakika wa namba

"Msimu uliopita kuna nafasi ilikuwa ikifahamika anacheza nani na mtu huyo anapokosekana inakuwa ni tatizo. Lakini msimu huu jambo hilo halitakuwepo. Wachezaji waliosajiliwa wote ni wazuri na kwa kweli hakutakuwa na mchezaji mwenye uhakika wa namba, kocha tu ndio ataamua," alisema Mukoko

Jambo hilo lilidhihiri kule Morocco kwani wachezaji walikuwa wakijituma kwelikweli mazoezini kila mmoja akipambana kumshawishi Nabi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
56m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’