Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amethibitisha kuwa kundi la pili la wachezaji waliokuwa wamesalia nchini Morocco, linaondoka mchana wa leo kurejea nchini tayari kwa kilele cha Wiki ya Mwananchi siku ya Jumapili
Aidha Mfikirwa amesema Zanaco Fc kutoka Zambia ambayo imealikwa kukipima kikosi cha Yanga, itawasili nchini leo
Katika hatua nyingine, wachezaji waliorejea nchini mwanzoni mwa wiki hii, jana walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya DTB mchezo uliopigwa Avic Town
Yanga iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 mabao ya Yanga yakifungwa na Kibwana Shomari, Ditram Nchimbi na Yannick Bangala wakati DTB ilifunga bao lake kupitia kwa Emmanuel Ngama
DTB inashiriki ligi daraja la kwanza ambapo hivi karibuni imewasajili wachezaji kama Juma Abdul na Amissi Tambwe