Kiungo Mukoko Tonombe leo amejumuika kwenye mazoezi ya kikosi cha Yanga yaliyoanza majira ya saa 1 usiku kwa saa za Morocco
Huko kwenye mitandao ya kijamii kumezushwa mengi kumuhusu Mukoko, hasa baada ya kutoonekana katika mazoezi ya Yanga yanayoendelea nchini Morocco
Pamoja na ufafanuzi uliotolewa na Yanga kuhusu kukosekana kwake, bado baadhi ya wanahabari tena wengine maarufu waliendelea kusambaza uzushi kuwa mchezaji huyo amegoma kufanya mazoezi baada ya Yanga kumzuia kujiunga na RS Berkane
Mukoko ni Mwananchi, mwenyewe amesema bado kuna kazi hajaikamilisha hivyo hawezi kuondoka bila ya kazi hiyo kukamilika...!



ADVERTISE HERE