Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wamepata ushindi wao wa pili kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuwachapa bao 1-0 mabingwa wenzao wa Zanzibar, JKU.
Mchezo huo uliokuwa mkali uliishuhudia Yanga ikipata bao lake kwenye dakika ya 90 mfungaji akiwa Hassan Kessy aliyefunga bao la 'kideoni' baada ya kupigiana 'kampa-kampatena' na Pius Buswita aliyemsogezea pasi kwa kisigino.
Yanga ingeweza kuongoza mapema tu kwenye kipindi cha kwanza kama nafasi mbili alizopata mshmabuliaji Matheo Antony angezitumia.
Kocha Msaidizi Shedrack Nsajigwa akishirikiana na mwenzake Noel Mwandila wameendelea kubadili kikosi kwa kuwapa nafasi vijana ili kuwapa uzoefu zaidi.
Mabadiliko waliyofanya kwenye kipindi cha pili kwa kuwaingiza Nkomola/Matheo, Said Musa/Juma Mahadhi, Raphael Daudi/Nadir Haroub, Ibrahim Ajib/Emanuel Martin na Geofrey Mwashiuya/Papy Tshishimbi yaliongeza uhai hasa alipoingia Ibrahim Ajib.
Yanga imefikisha alama sita sawa na Mlandege na Singida United.
Yanga itashuka tena dimbani kesho Januari 05, 2018 kuivaa Taifa ya Jan'gombe mchezo unaotarajiwa kuanza saa mbili na nusu usiku.

ADVERTISE HERE