Mwamba anatambulishwa hukohuko Morocco

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Aug 2021
Mwamba anatambulishwa hukohuko Morocco

Yanga iko nchini Morocco leo ikianza maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya michuano ya Kimataifa

Miongoni mwa wachezaji watakaokuwa sehemu ya kikosi kilichoingia kambini ni beki kiraka Yannick Bangala Litomba

Kitasa huyu ametua kwa Wananchi akitokea klabu ya FAR Rabat inayoshiriki Ligi Kuu hapo Morocco. Bangala ameungana na wenzake hapohapo Morocco

Ndiye mchezaji pekee ambaye utambulisho wake bado haujawa rasmi

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Bangala atatambulishwa huko huko Morocco kwani taratibu za usajili wake zilikamilika mapema akiwa miongoni mwa wachezaji watakaoitumikia Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

Pamoja na kumudu vyema nafasi ya ulinzi wa kati, beki huyo aliyewahi kuzitumikia AS Vita na DC Motema Pembe zote za DR Congo, pia anamudu kucheza kama mlinzi wa upande wa kulia na kiungo mkabaji

Kwa nyakati tofauti aliitwa timu ya Taifa ya DR Congo na alitumika zaidi kama mlinzi wa kati au kiungo mkabaji

Ni mchezaji mwenye uzoefu wa michuano ya Kimataifa, akiwa na umri wa miaka 27

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’