Hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi kuelekea msimu wa 2021/22 itafanyika visiwani Zanzibar August 22 2021
Wiki ya Mwananchi inabeba siku saba za Wanachama na Mashabiki wa Yanga kujitolea kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii
Kilele cha wiki hiyo ni August 29 kwa tukio kubwa la utambulisho wa kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano
Tukio hilo litahitimishwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa kwa kikosi cha Yanga kushuka uwanjani kuikabili timu alikwa ambayo itakuwa imekaribishwa kusherehesha siku hiyo
Yanga itashuka dimbani siku hiyo ikiwa imetoka kambini nchini Morocco
ADVERTISE HERE