Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza ni miongoni mwa wachezaji waliopatiwa chanjo ya virusi vya corona Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo
Ntibazonkiza anatarajiwa kujumuishwa katika msafara wa wachezaji watakaoelekea kambini nchini Morocco hapo kesho
Zoezi la chanjo lilifanyika kwa wachezaji wote wa Yanga ambao hawakupatiwa chanjo hiyo awali
Kikosi cha Yanga kitaondoka jijini Dar es salaam mapema kesho Jumapili kuelekea Morocco ambako wataweka kambi ya siku 11

ADVERTISE HERE