Msuva ampa moyo Mahadhi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jan 2018
Msuva ampa moyo Mahadhi
Baada ya winga wa Yanga Juma Mahadhi kuandika waraka wa kuwaomba rambi viongozi na mashabiki wa Yanga juu ya kutofikia matarajio yao na kuahidi kubadilika na kutimiza wajibu wake ipasavyo, winga wa zamani wa Yanga Simon Msuva amepongeza hatua hiyo ya Mahadhi.

Msuva amesema kitendo cha Mahadhi kutambua mapungufu yake ni matua kubwa kuelekea mafanikio. Jambo la msingi kwake ni kuhakikisha anajituma na kutimiza yale yote anayowajibika nayo.

Aidha Msuva amemtabiria Mahadhi kuwa kama ataongeza bidii na kujituma zaidi atafika pale alipo yeye na pengine zaidi yake.

"Neno Msamaha , Nisamehe sio Ujinga muhimu umejua wapi umeteleza Naimani Unakipaji kikubwa sana Endelea kuamini kwamba unaweza," amefunguka Msuva kupitia ukurasa wake wa Instagram.

"No time to waste Brother Hongera kwa kutambua ilo naimani wewe ni Champion Endeleza mapambano Mdogo wangu usonge mbele uje ufike Nilipo na Zaidi Nafasi bado Unayo @jumamahadhi21 Twende tuisogeze Tanzania Yetu."

Mahadhi alitarajiwa kuziba pengo la Msuva mwanzoni mwa msimu baada ya winga huyo mkali wa mabao kusajiliwa na Difaa Al Jadida ya Morocco.

Msuva amerejea nchini kwa mapumziko ya wiki moja baada ya ligi kuu ya Morocco kusimama.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’