Bangala ndiye mrithi wa Lamine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Aug 2021
Bangala ndiye mrithi wa Lamine

Beki kisiki wa timu ya Taifa ya DR Congo Yannick Bangala Litombo yuko nchini kumalizana na Yanga, imefahamika

Bangala ametokea Morocco ambako alikuwa akiitumikia klabu ya FAR Rabat ambayo ilimaliza katika nafasi ya tatu msimu wa ligi uliomalizika

Beki huyo pia amewahi kuitumikia klabu ya AS Vita, kuna wakati Yanga ilijaribu kumsajili wakati akiwa AS Vita pasipo mafanikio

Imeelezwa Bangala alishafikia makubaliano binafsi na Yanga na pengine beki huyo anasubiri utambulisho tu

Wachezaji kutoka DR Congo wanavutiwa kujiunga na Yanga kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo

Lakini pia mishahara minono wanayolipwa wachezaji, inawavuta wengine kutoka kila pembe ya Afrika

Bangala ni mchezaji mwenye uzoefu katika michuano ya Kimataifa, akicheza timu ya Taifa, michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho

Wakala wa mchezaji huyo Faustino Mukandila ambaye pia ni wakala wa Shabani Djuma, ndiye aliyefanikisha ujio wake nchini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’