Imebainika kuwa winga Tuisila Kisinda anayekwenda kujiunga na RS Berkane ya Morocco atalipwa mshahara wa takribani Tsh Milioni 34 kwa mwezi
Aidha nyota huyo atavuna kitita cha Tsh Milioni 350 kutoka kwenye dau la usajili lililowekwa mezani na RS Berkane
RS Berkane wanatajwa kuweka mezani dau la dola laki nne, ambapo dola 150,000 zitaingia kwenye akaunti ya Kisinda na zilizobaki (zaidi ya Mil 500) zitaingia kwenye akaunt ya Yanga
RS Berkane pia wametoa dola 100,000 kugharamia kambi ya Yanga itakayowekwa nchini Morocco
Uongozi tayari umethibitisha kikosi kitaondoka nchini kuelekea Morocco kwa ajili ya kambi
ADVERTISE HERE