Injinia Hersi athibitisha ofa ya Kisinda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Aug 2021
Injinia Hersi athibitisha ofa ya Kisinda

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said amekiri kuwa Yanga imepokea ofa kutoka klabu ya RS Berkane kumtaka winga Tuisila Kisinda

Aidha Hersi amesema sio Kisinda tu, wapo wachezaji wengine ambazo ofa zao ziko mezani zikiendelea kufanyiwa tathmini

Hersi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano amesema isichukuliwe kama ni jambo baya pale wachezaji wanapotakiwa na timu nyingine

"Ni kweli tumepokea ofa kutoka RC Berkane kwa ajili ya Kisinda. Lakini sio yeye peke yake, tuna ofa kwa ajili ya Yacouba Songne na Mukoko Tonombe pia. Tunaendelea kuzifanyia tathmini kama kuna mwafaka utafikiwa tutatoa taarifa," alisema Hersi

"Yapo mazingira ambayo yanaweza kupelekea mchezaji akauzwa mfano gharama za kuuza mchezaji, muda wa mkataba wake uliobaki na pia kuangalia kama sokoni kuna mbadala wake."

"Suala la kuuza wachezaji linafanyika sana duniani na ni muhimu nasi kwenda katika njia hiyo ambayo wenzetu wanakwenda."

Yanga inahusishwa na winga mwingine kutoka AS Vita Jesus Moloko kuchukua nafasi ya Kisinda

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’