Siwa akerwa na waamuzi Kagame Cup

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Aug 2021
Siwa akerwa na waamuzi Kagame Cup

Kocha wa Yanga Razak Siwa amesema kumekuwa na changamoto ya waamuzi kwenye michuano ya kombe la Kagame inyaoendelea jijini Dar es salaam

Juzi baada ya mchezo kati ya Yanga dhidi ya Atlabara ambao ulimalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana, Siwa alieleza masikitiko yake kwa waamuzi kushindwa kutafsiri vyema sheria 17 za mchezo wa soka

"Timu yangu ilicheza vizuri lakini sikufurahishwa na maamuzi ya mwamuzi sababu ametunyima penalti za wazi kabisa, hili si jambo zuri sababu klabu imetumia gharama kubwa kuiandaa timu halafu mtu mmoja anakwenda kufanya vitu vya hivyo," alisema Siwa

Mkufunzi huyo wa makipa amesema katika mchezo wao wa ufunguzi mambo kama hayo yalitokea, lakini wakachukulia kama ni makosa ya kibinadamu, lakini ameshangazwa kuona jambo hilo likajitokeza tena kwenye mchezo wao wa pili.

Siwa amesema Yanga inaona fahari kushiriki michuano hiyo, lakini ipo haja ya waandaaji Cecafa kuwa makini katika uteuzi wa waamuzi wanaochezesha michuano hiyo ili kuondoa  malalamiko ambayo yanaharibu maana halisi ya michuano hiyo

Yanga itashuka dimbani kesho Jumamosi kukamilisha hatua ya makundi kwa kuikabili Express katika mchezo ambao Yanga inahitaji ushindi ili kutinga nusu fainali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’