Mastaa wa zamani wa Yanga wamekiri kuumizwa na kipigo cha mabao 2-0 kutoka Mbao, lakini wamewapa moyo vijana wao kuwa wakaze tu, kwani bado wana nafasi kubwa ya kutetea ubingwa msimu huu.
Sekilojo Chambua, Henry Morris na Abeid Mziba ‘Tekelo’ kwa nyakati tofauti walisema Yanga haina haja ya kupaniki na badala yake waelekeze nguvu zao katika Kombe la Mapinduzi na wakirudi wawe wameiva kuweza kufanya kweli katika ligi.
Chambua alisema kwa uzoefu alionao katika ligi, anajua namna wachezaji na mashabiki wanavyoumia kwa kulinganisha matokeo yao na watani zao Simba, lakini bado hawapaswi kukata tamaa.
“Benchi la Ufundi lisahaulishe wachezaji kipigo cha Mbao na kuelekeza nguvu katika mashindano yaliyopo mbele yao ikiwamo Mapinduzi na Ligi ya Mabingwa Afrika na hata mechi zao zilizosalia za Ligi Kuu,†alisema.
Naye Mziba alisema ligi bado ndefu, hivyo haoni sababu ya wachezaji kuumia na kuona wameishashindwa vita.
“Wachezaji wanapaswa kutambua kwamba wapo vitani, matokeo hayo yawatie moyo kwa kujipanga zaidi badala ya kunyosheana vidole,†alisema Mziba.
Kwa upande wa Morris alisema safu ya ulinzi ya Yanga haikuwa na mawasiliano hivyo kuruhusu mabao, lakini bado Yanga ina kikosi kizuri na kama itajipanga kwa mechi zijazo itatetea taji lake kwa mara ya nne mfululizo.
Kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Ally Yusuf ‘Tigana’ alisema tatizo la klabu kongwe ni kutopenda kufungwa, lakini ukweli soka ndivyo lilivyo na Yanga ijipange tu bila kujali kama wameachwa pointi tano na Simba.
Yanga ilikumbana na kipigo hicho cha tatu mfululizo katika mechi zake dhidi ya Mbao za kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Msimu uliopit a ilifunga mara mbili kwa bao 1-0 katika nusu fainali ya Kombe la FA na mechi ya mwisho ya ligi.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE