Tulizidiwa - Nsajigwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jan 2018
Tulizidiwa - Nsajigwa
Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amekiri kuwa Mbao FC ilistahili kupata ushindi baada ya kuzitumia vyema nafasi walizotengeneza.

Yanga ilifunga mwaka 2017 vibaya kwa kuchapwa mabao 2-0 na Mbao FC katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la CCm Kirumba, Disemba 31.

Nsajigwa anayesaidiana na Noel Mwandila kukinoa kikosi cha Yanga baada ya kocha Mkuu George Lwandamina kupata msiba, amesema katika kipindi cha kwanza timu zilitoshana nguvu lakini Mbao Fc walifanya vizuri zaidi kwenye kipindi cha pili.

"Hali ya mchezo kwa ujumla ilikuwa nzuri kiasi chake, kipindi cha kwanza mechi ilikuwa nusu kwa nusu lakini kipindi cha pili kilibadilika, Mbao walibadilika wakaja juu badae wakapata nafasi wakazitumia," amefunguka Nsajigwa

"Mpira ni mchezo wa matokeo, usipobadili nafasi ulizopata kuwa magoli basi huwezi kufunga"

"Tumepoteza mchezo tunawapa hongera Mbao wamefanya kazi yao vizuri wamepata ushindi."

Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Yanga msimu huu na sasa izitumie vyema wiki mbili za michuano ya kombe la Mapinduzi kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo huo.

Yanga pia inakabiliwa na michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika inayoanza mwezi ujao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’