Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga Injinia Hersi Said alisema msimu huu wamekusudia kuja na utaratibu tofauti wa uambulisho wa wachezaji wapya
Msimu uliopita wachezaji walikuwa wakitua uwanja wa Ndege na Wananchi kwenda kuwapokea
Pengine msimu huu GSM watakuja na utaratibu wenye manufaa ya kibishara kwa GSM na Yanga
Uzinduzi wa jezi mpya ni jambo muhimu ambalo linapaswa kwenda sambamba na utambulisho wa wachezaji wapya
Wananchi wanaipenda timu yao na ndio maana Yanga imeendelea kukimbiza katika mauzo ya jezi
Kuchelewa kwa uzinduzi wa jezi ni kosa ambalo halipaswi kurudiwa kama ilivyokuwa msimu uliopita
Msimu uliopita Yanga ililazimika kucheza mechi yake ya kwanza ya msimu mpya wakitumia jezi za msimu wa nyuma yake
GSM wajipange, washushe jezi kabla ya tukio la wiki ya Mwananchi ikiwezekana wazitambulishe mapema wakati watakapokuwa wakitambulisha wachezaji wapya
Yaani inapotangazwa mchezaji amesajiliwa, jezi yake iwe tayari inapatikana pale dukani Jangwani na maduka yote ya GSM pamoja na Mawakala wao
Huko nchi za wenzetu hasa barani Ulaya sehemu ya gharama za usajili wanazirudisha kupitia mauzo ya jezi