Wananchi wamekamilisha msimu kwa kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri, Dodoma
Ulikuwa mchezo wa kukamilisha ratiba kwa timu zote, Yanga ikiwa imejihakikishia kumaliza katika nafasi ya pili
Katika mchezo wa leo kocha Nasreddine Nabi alifanya mabadiliko ya kikosi chake akiwapumzisha baadhi ya wachezaji wake muhimu
Yanga sasa inaelekeza nguvu zake kwenye mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Simba ambao utapigwa Julai 25 mkoani Kigoma

ADVERTISE HERE