Ofa zamiminika kumtaka Yacouba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2021
Ofa zamiminika kumtaka Yacouba

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga Injinia Hersi Said amesema wamepokea ofa kadhaa kutoka timu mbalimbali zinazomuhitaji mshambuliaji Yacouba Songne

Hersi amesema mchezaji huyo amekuwa katika kiwango bora akiwa chachu ya mafanikio ya kikosi cha Yanga kwenye mechi za hivi karibuni

Hersi amesema hiyo inaonyesha ni kwa kiasi gani nyota waliowasajili msimu uliopita wameonyesha thamani yao katika kikosi cha Yanga pamoja na kuwa wapo wachache walioshindwa kutamba

"Tuna ofa nyingi zinazomuhitaji Yacouba, utaona ni kwa kiasi gani ameweza kuonyesha thamani yake ndani ya kikosi mpaka timu hizo kumuona. Niseme kwa kiasi kikubwa usajili wetu wa msimu huu ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa. Tulileta wachezaji bora pamoja na kuwa wapo wachache wameshindwa kuonyesha uwezo wao"

"Tumedhamiria kufanya maboresho makubwa ili kuhakikisha msimu ujao tunakuwa na timu imara zaidi," alisema Hersi

Haitakuwa rahisi kwa Yanga kumuuza Yacouba kwani mabingwa hao wa kihistoria wana malengo ya kufanya vizuri katika michuano ya msimu ujao

Yanga inatarajiwa kusajili washambuliaji wengine wenye ubora wa Yacouba au zaidi ili kuhakikisha malengo yanafanikiwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’