Klabu ya Yanga na Azam Media wamesaini mkataba wa makubaliano ya haki za matangazo wenye thamani ya Tsh Bilioni 34.8 (Bil 41 na VAT) kwa miaka 10
Makubaliano hayo yanawapa Azam Media haki za kusimamia na kuandaa maudhui yanayohusiana na Yanga, ikiwemo Yanga TV, kuonyesha mechi zote za Yanga iwe kirafiki au Kimataifa, mazoezi, mahojiano na mengineyo
Yanga italipwa fedha zake kila mwezi katika kipindi chote cha miaka 10 ambapo watalipwa kati ya Tsh Milioni 200 mpaka 360
Aifsa Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando amesema makubaliano hayo yamefikiwa baada ya majadiliano ya uongozi wa Yanga ambapo kiwango cha pesa kimeendana na thamani ya klabu
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hoteli ya Serena, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla ameipongeza Azam Media kwa kuendelea kuboresha mazingira ya soka la Tanzania
Amesema Yanga watatimiza masharti yote ya mkataba huo huku akiwataka Wanachama na mashabiki kuunga mkono makubaliano hayo