Nabi anasuka Yanga ya Kimataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jul 2021
Nabi anasuka Yanga ya Kimataifa

April 23 2021 ulikuwa mchezo wake wa kwanza tangu akabidhiwe mikoba ya kukinoa kikosi cha Yanga akipokea kijiti kutoka kwa kocha wa muda Juma Mwambusi

Ilikuwa dhidi ya Azam Fc, akipoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0 pale uwanja wa Benjamin Mkapa

Sio matokeo yaliyowafurahisha Wanayanga wengi, lakini Nabi akawaambia watulie, baada ya muda kila kitu kitakuwa sawa

Tangu wakati huo Yanga haikupoteza tena mchezo wowote kwenye ligi na hata FA

Mchezo pekee waliokosa alama zote tatu ni dhidi ya Namungo Fc ambao kila mmoja anafahamu mshika kibendera aliwanyima Yanga ushindi

Waliokuwa wakiibeza Yanga kabla ya mchezo dhidi ya Simba hawakufahamu kazi kubwa aliyokuwa ameifanya Nabi kukiimarisha kikosi chake

Wakati wanakwenda kumpasua Simba, mabingwa hao wa kihistoria walitoka kushinda mechi tano mfululizo, ushindi dhidi ya Simba ulikuwa wa sita

Nabi ameiongoza Yanga katika jumla ya michezo tisa, ushindi saba, sare moja na kupoteza mchezo mmoja

Kikosi ni kilekile ambacho wengi waliamini kina wachezaji wa kawaida sana, Nabi amekibadilisha kuwa timu isiyofungika

Ni wazi kwa usajili ambao Yanga wanafanya, ukiwa na baraka za Nabi kwa asilimia 100, msimu ujao Yanga itakuwa imara zaidi

Kocha huyu raia wa Tunisia amewahi kushinda taji ya CAF CC mwaka 2012 akiwa na AC Leopards na amedhamiria kurejea mafanikio hayo akiwa na Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11m ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
34m ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
4h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
8h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’