Kiungo wa Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenya, Kenneth Muguna, anahusishwa kutakiwa na mabingwa wa kihistoria, Yanga
Tetesi za fundi huyu wa mpira kutakiwa na Yanga, zilianza kuvuna tangu juzi baada ya mtandao wa Goal kuthibitisha kuwepo kwa mazungumzo kati ya Wakala wa mchezaji huyo na Yanga
Yanga ilijaribu kumsajili Muguna dirisha la usajili lililopita lakini ilishindikana baada ya Gor Mahia kutaka dau kubwa
Mkataba wake na Gor Mahia ulimalizika Juni 30 na hivyo nyota huyo sasa yuko huru
Yanga inasaka mbadala wa mkongwe Haruna Niyonzima ambaye nafasi yake imeendelea kuwa finyu kwenye kikosi
Muguna amekuwa mchezaji muhimu wa Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenya juzi akiisaidia Gor Mahia kupata ushindi wa mikwaju ya penati 4-1 dhidi ya AFC Leopards katika mchezo wa fainali ya kombe la FKF
Awali Yanga ulikuwa ikihusishwa kumuwania kiungo wa Meneama Mcongomani Merceil Ngimbi Vundi ambaye hata hivyo TP Mazembe walimtambulisha jana baada ya kufanikiwa kumsajili
Aidha, mabingwa hao wa kihistoria jana walithibitisha kumsajili nahodha wa AS Vita Shabani Djuma
Wananchi wamepania kusajili wachezaji wa daraja la juu ambao wataongeza chachu kwenye mapambano kuwania ubingwa msimu ujao pamoja na michuano ya Kimataifa