Shamra shamra za wachezaji wa Yanga baada ya ushindi dhidi ya Simba jana ziligubikwa ya taswira ya kipekee
Wachezaji walishangilia sana ushindi baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha kumaliza mchezo
Ulikuwa ushindi muhimu dhidi ya watani wa jadi, ushindi ambao uliwakata ngebe Simba
Aidha kauli alizotoa msemaji wa Simba Haji Manara siku chache kabla ya mchezo kwa kuwadharau wachezaji wa Yanga, malipo yake ni kipigo
Wachezaji walikuwa na dukuduku katika mioyo yao, walimaliza machungu kwa 'kuwachapa'
Unapozungumzia timu yenye historia kubwa katika soka la Tanzania lazima uwe na adabu...!
ADVERTISE HERE