Sasa ni rasmi watani wa jadi Yanga na Simba wataumana kwenye mchezo wa fainali michuano ya kombe la FA baada ya Simba nao kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam Fc
Hii ni mara ya kwanza Yanga na Simba zinakutana kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Lakini pia itakuwa mara ya kwanza mchezo huo wa watani kupigwa nje ya jiji la Dar es salaam
Jana Yanga ilitangulia fainali baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United
Watani hao wa jadi pia watakutana mara mbili mwezi Julai
Mchezo wa kwanza ni wa ligi kuu ambao utapigwa Julai 03
Hizi ni mechi mbili muhimu sana kwa kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi kuhakikisha kikosi chake kinapata matokeo mazuri hasa kushinda kombe la FA
ADVERTISE HERE