Kocha wa zamani wa Yanga Cedric Kaze amewapongeza wachezaji kwa kuweza kutinga fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Jana Yanga liichapa Biashara United bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora
Kaze amesema amafanikio waliyopata Yanga yamechangiwa na uvumilivu wao
"Kadiri unavyosubiri jambo, ndivyo utakavyolithamini litakapofika. Safi sana...!," aliandika Kaze kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Kaze aliinoa Yanga kwa takribani miezi mitano kabla ya kuondolewa na nafasi yake kushikiliwa kwa muda na kocha Juma Mwambusi ambaye alikuja kumpisha kocha aliyepo sasa, Nasreddine Nabi
ADVERTISE HERE