Juzi Kocha Edna Lema aliachana na Yanga Princess baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa Yanga kuvunja makataba wake
Lema aliinoa Yanga Princess kwa misimu miwili ambapo msimu uliomalizika nusura atwae ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite' kama sio watani zao Simba Queens kushinda mchezo dhidi ya Baobab Queens kwa kufunga bao kwenye dakika ya 98!
Imefahamika kuwa Lema huenda akaibukia nchini Zambia katika klabu ya Wanawake ya Zesco United
Kwa wasiofahamu, Lema ni kocha aliyehitimu mafunzo ya CAF daraja B, vyeti vyake vinamruhusu kufundisha hata klabu ya Ligi Kuu
Kama mpango wake wa kutua Zambia utafanikiwa, atakuwa kocha wa kwanza Mwanamke kupata nafasi ya kwenda kufundisha soka nje ya nchi
Pamoja na kuwa bado Wananchi walikuwa wakimuhitaji, hii ni fursa kubwa sana kwake ambayo sio rahisi kuiachia..!