Yanga, TFF wayamaliza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jun 2021
Yanga, TFF wayamaliza

Mgogoro kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu ya Yanga umefikia kikomo baada ya Serikali kuzikutanisha pande zote mbili na kila mmoja kutoa dukuduku lake

Kikao hicho kimeitishwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuongozwa na katibu mkuu wake, Dk Hassan Abbas lengo likiwa kumaliza tofauti juu ya pande hizo mbili katika masuala mbalimbali ambayo yalikuwa hayaendi sawa na kuleta sintofahamu ambayo ilikuwa inaharibu taswira ya mpira nchini

Viongozi waliohudhuria kwa upande wa Yanga ni Katibu Mkuu, Haji Mfikirwa na Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla wakati kwa TFF iliwakilishwa na viongozi wake wa juu.

Katika mahojiano yake na gazeti la Serikali la HabariLeo, Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo nchini, Dk Singo amekiri kufanyika kwa kikao hicho jana, lakini walikubaliana kuwa Yanga na TFF ndio watakuwa wazungumzaji wa muafaka huo.

Dk Singo alisema kuwa viongozi wa Yanga na TFF ndio watatoa taarifa kamili ya kikao hicho ambacho kilifanyikia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

"Ni kweli tulikuwa na kikao na viongozi wa Yanga pamoja na TFF, lakini ninachoweza kukwambia ndugu mwandishi, mambo yamekwenda sawa ispokuwa tulivyokubaliana kuwa wahusika wakuu, ambao ni Yanga na TFF ndio watatoa taarifa kupitia midandao yao ya kijamii," alisema Singo.

Awali, Serikali ilitangaza kuzikutanisha pande hizo mbili kutokana na uongozi wa klabu ya Yanga kupeleka malalamiko yao kwa Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa wakidai kubaguliwa na TFF katika mambo mbalimbali.

Baadhi ya madai yao ni uongozi wa TFF kushindwa kuzitolea maamuzi baadhi ya kesi ambazo wamekuwa wakizilalamikia.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Mfikirwa amekiri kikao hicho kufanyika chini ya usimamizi wa Serikali na pande zote kufikia muafaka kwa faida ya soka la Tanzania

Mfikirwa alisema taarifa kamili wataitoa baadaye kupitia mitandao, lakini maamuzi ya kikao hicho anaamini yatakuwa na tija kwa klabu yao ambayo imepambana kwa muda mrefu kutafuta haki zao za msingi.

"Nashukuru Serikali imetimiza ahadi yake ya kutukutanisha na uongozi wa TFF, na kueleza yale malalamiko yetu na pia nafurahi kuona muafaka umefikiwa kwa maslahi mapana ya mpira wa Tanzania, "alisema Mfikirwa

HabariLeo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’