Achana na dhurma waliyofanyiwa Yanga U20 kwenye mchezo wa fainali jana dhidi ya Mtibwa Sugar kwa bao lao halali kukataliwa na mwamuzi msaidizi aliyeshindwa kutafsiri vyema sheria ya kuotea, vijana wa kocha Said Maulid wanastahili pongezi kwa vile walivyopambana katika michuano ya mwaka huu
Licha ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1, Yanga U20 waliteka 'shoo' kwenye kipindi cha pili
Mlinda lango wa Yanga U20 Godfrey Magaigwa amechaguliwa kuwa kipa bora wa ligi kuu ya vijana
Magaigwa alikuwa bora sana katika michuano hiyo, ni tuzo aliyostahili
Kocha wa makipa Razack Siwa hapaswi kuchelewa kumpandisha kinda huyu kwenye timu ya wakubwa
Magaigwa aliifanya mazoezi na timu ya wakubwa wakati wa mapumziko ya michuano ya Kimataifa
Aidha mlinzi wa kati Ally Said amechaguliwa kuwa beki bora wa mashindano. Hii ni hazina nyingine ya Yanga kwenye safu ya ulinzi
Nyota wengine waliofanya vizuri sana kwenye michuano hiyo Abdulkarim Yunus aliyefunga mabao manne na Omary Chibada aliyen'gara eneo la kiungo
Yunus na Chibada wametumika mara kadhaa kwenye timu ya wakubwa